Hakika Mtume wa Uislaam (s.a.w) aliupatia ulimwengu Zawadi yenye thamani
kubwa na ya aina ya pekee, na ndani ya Zawadi hiyo mna Saada na mafanikio kwa
wanadamu wote, nayo ni Nidhamu, Hukumu na Kanuni mbali mbali alizo zithibitisha
na kuwawekea Waislaam. Na kanuni hizo ni miongoni mwa kanuni na hukumu bora
kabisa na zisizo na upungufu wa aina yoyote katika ulimwengu huu. Ili kuyajua
hayo someni kwa jicho la udadisi mwenendo na historia yake (s.a.w) ili muweze
kuona mamia kwa maelfu ya mifano mizuri ambayo lau kama itakusanywa yote kwa
pamoja katika sehemu moja, mtu yeyote asie kuwa Muislaam hata kama atakuwa na
asabia ya dini yake ataweza kuathirika na mifano hiyo na kuamua kujiunga na
Uislaam (Kusilimu).
Kwa hivyo basi ikiwa itawezekana katika ulimwengu wa leo kufuatwa na kutekelezwa
mfumo na wa Mtume mtukufu (s.a.w), na pia mfumo sira ya Amirul-muuminiin Ali bin
Abi Twaalib (a.s) katika majumba yetu, sehemu zetu za kazi, katika mashirika,
katika nchi zetu na miji yetu, kwa hakika yange thibitika yaliyo thibitika
ulimwenguni kabla ya miaka 1400 iliyo pita, na hii ndio taawili (Tafsiri) ya
kauli yake Mwenyezi Mungu alie takasika isemayo:
(ورأيت الناس يدخلون في دين الله أفواجا)
(Na utawaona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi)
Na mtaona ya kuwa watu maelfu kwa maelfu kama si mamilioni watakuwa wakiingia
katika dini ya Uislaam.